Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni dhidi ya homa ya manjano DRC na Angola yaendelea vyema

Kampeni dhidi ya homa ya manjano DRC na Angola yaendelea vyema

[caption id="attachment_292762" align="alignleft" width="350"]dailynews168b-16

Kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya manjano huko Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambayo ilianza tarehe 16 mwezi huu inaendelea vyema huku mwitikio ukielezwa kuwa ni mkubwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema ikiwa leo ni siku ya nne ya kampeni hiyo zaidi ya watu zaidi ya milioni Tano wamepatiwa chanjo kwenye mji mkuu wa DRC Kinshasa na viunga vyake, idadi ambayo ni sawa na zaidi ya asilimia 70 ya jamii inayolengwa.

Na kuhusu Angola, msemaji wa WHO Tarik Jasarevic anasema kampeni inaendelea mpakani na DRC na kwamba..

(Sauti ya Tarik)

Hadi sasa watu zaidi ya milioni Moja wamepatiwa chanjo na hii ni sawa na theluthi mbili ya jamii iliyolengwa nchini Angola.”