Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya kibinadamu yaongezeka Nigeria:IOM/WFP

Mahitaji ya kibinadamu yaongezeka Nigeria:IOM/WFP

Eneo la bonde la ziwa Chad lililoghubikwa na machafuko ya Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria linashuhudia mtafaruku mkubwa wa masuala ya ulinzi na ongezeko la wakimbizi wa ndani. Rosemary Musumba na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ROSE)

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, Nigeria pekee watu zaidi ya milioni 2.2 ni wakimbizi wa ndani, ikijumuisha wengi wanaosihi kwenye makazi ya muda, bila kupata huduma za msingi , na idadi hiyo inaongezeka haraka.

WFP inasema kuzorota kwa uchumi kunaweza kushuhudia idadi hiyo kuongezeka, huku tathimini ya chakula ya shirika hilo ikionya kwamba bei kcha chakula katika maeneo yaliyoathirika inaongezeka.Bettina Luescher ni msemaji wa WFP.

 

(SAUTI YA BETTINA) (ATASOMA FLORA)

 “Idadi mpya ya watu wanaohitaji msaada Kaskazini Mashariki mwa Nigeria sasa imeongezeka hadi milioni 4.5, na tunahofia itaongezea milioni moja nyingine. Watu wetu walioko huko wanahofia kwamba hadi sasa hatuna fursa ya kutosha kuweza kuwapata watu wengi zaidi wanaoteseka.”