Usaidizi wafika Bama na hali inatia matumaini- Lanzer

22 Agosti 2016

Huko Bama, kwenye jimbo la Borno, kaskazini-mashariki mwa Nigeria, mji uliokuwa umeharibiwa zaidi na machafuko sasa kuna maendeleo ikilinganishwa na mwezi Aprili nilipotembelea.

Hiyo ni kauli ya msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa ukanda ya Sahel, Toby Lanzer aliyotoa baada ya ziara yake ya siku tano kwenye eneo hilo hivi karibuni, ikiwa ni ziara yake ya pili.

Mathalani amesema shule zimefunguliwa, sambamba na kliniki ambazo sasa zinatoa matibabu kwa wagonjwa.

Na zaidi ya hapo Bwana Lanzer amesema cha kuridhisha ni kuona pia vijana wa Bama waliokuwa wamekimbilia Maidguri, wamererejea na wanasaidia mashirika ya misaada kuendeleza kazi za usaidizi kwa watu 20,000 wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi wa ndani.

Hata hivyo Bwana Lanzer amesema bado usaidizi unahitajika Bama na kwenye miji mingine ya majimbo ya Adamawa, Borno na Yobe.

Mzozo unaosababishwa na waasi wa kikundi cha Boko Haram huko Nigeria umesababisha watu takriban milioni tisa wanahitaji msaada wa dharura ambapo milioni nne na nusu ya watu hao wanahitaji chakula na waliosalia wamekimbia makazi yao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter