Ban aipongeza Brazil, IOC kwa mashindano ya Olimpiki 2016:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameinpongezi nchi ya Brazil, jiji la Rio De janeiro,Wananchi wa Brazil,kamati ya maandalizi ya ndani ya olimpiki na pia kamati ya maanadalizi ya kimataifa kwa kuandaa olimpiki yenye fanaka iliyoifika tamati hapo jana.
Ban alishiriki hapo awali sherehe za ufunguzi ya michezo hiyo na pia kuwatembelea timu ya wakimbizi ya olimpiki katika makaazi ya wanamichezo. Katibu Mkuu ameshukuru raia wa Brazil kwa ukarimu wao na ulimwengu wa michezo katika kuandaa michezo ya olimpiki ambayo ilikuwa ya kwanza kuandaliwa bara la Amerika kusini na akawahimiza washikadau kuchukua fursa ya kuchangia katika maendeleo endelevu kutokana na yale yaliyoletwa na kuandaliwa kwa michezo hiyo.