Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kesi ya kihistoria ICC:

Ban akaribisha kesi ya kihistoria ICC:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameikaribisha kesi ya kihistoria toka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC), inayomkabili ya Bw. Ahmed  Al Mahdi anaetuhumiwa kwa kesi ya uhalifu wa kivita, dhidi ya sanamu na majumba ya makumbusho huko Timbuktu, Mali mnamo mwezi july mwaka 2012.

Hii ni mara ya kwanza mahakama hii kumfikisha kizimbani mtuhumiwa kwa kosa la kusababisha hasara kwenye makumbusho au sehemu ya kuhifadhi utamaduni. Ban amesema inatia moyo sana, pia inatakiwa kufuatilia kwa karibu tabia iliyosheheni kila mahali dunia ambapo watu kwa makusudi wanaharibu sehemu za makumbusho na utamaduni wanapokuwa katika hali ya kivita.

Mashambulizi ya makumbusho ni utovu wa nidhamu kwa kazi kubwa iliofanywa na waliotutangulia na pia upoteshwaji wa misingi ya historia ya utamaduni wetu. Katibu Mkuu amekemea vikali  tabia hii na kuwataka watuhumiwa wa makosa haya kuchukuliwa hatua kisheria mara moja. Pia ameipongeza mahakama kuu ya kimataifa kwa utendaji wake na kuitaka itende haki na uwaajibikaji kwa watuhumiwa.