Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya homa ya ini kutokomezwa Afrika ifikapo 2030:WHO

Virusi vya homa ya ini kutokomezwa Afrika ifikapo 2030:WHO

Ifikapo mwaka 2030 , bara la Afrika linataka kutokomeza virusi vya homa ya ini kama moja ya tishio kubwa la afya barani humo. Hamasa hiyo ni baada ya shirika la afya duniani WHO kuzindua waraka unaojikita katika kuzuia, kuhudumia na kutibu homa ya ini Afrika, ikiwa ni muongozo wa ,kuchukua hatua kati yam waka 2016 hadi 2020.

WHO inasema lengo ni kuzipa muongozi nchi wanachama barani Afrika wa jinsi ya kutekeleza mkakati wa kwanza kabisa wa kiafya kuhusu homa ya ini, mkakati ambao ulipitishwa na baraza la afya duniani mwezi Mai mwaka jana. Duniani kote watu milioni 400 wameambukizwa homa ya ini aina B na C ikiwa ni mara kumi Zaidi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV.Frank Lule, Mkurugenzi Mkuu wa wa Kikanda Afrika..

(SAUTI YA DR Lule)

"Kikubwa zaidi sasa ni kuongeza uchunguzi na upimaji wa virusi vya hepatitis, na pia kuanzisha mpango wa matibabu, sio nchi nyingi ambazo zimeongeza matibabu ya virusi vya hepatitis, na hii ni moja ya mikakati ambayo itaongezwa katika nchi miaka mitano ijayo, na tunakata nchi ziwe na mikakati ya kitaifa ambayo itatumika kama chombo cha utetezi na uhamasishaji wa rasilimali"