Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari wa UNSOM wa tunzwa kwa huduma Somalia:

Askari wa UNSOM wa tunzwa kwa huduma Somalia:

Vikosi vya askari wa Umoja wa Mataifa wanao hudumia nchini Somalia (UNSOM) na Ofisi ya msaada nchini Somalia (UNSOS) wametunukiwa medali katika  sherehe  maalum kwa ajili ya huduma zao nchini humo. Brian Lehander na taarifa kamili..

(TAARIFA YA BRIAN).

Wafanya kazi hao 17 ambao ni wanajeshi, polisi na maafisa wa magereza walipata tuzo maalum la Umoja wa Mataifa zilizokabidhiwa na kutoka mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja nchini humo  Michael Keating, katika sherehe iliyofanyika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu .

Bwana Keating aliwashukuru wafanyakazi hao kwa ushujaa wao wa kufanya kazi katika mazingira magumu na kusema huu ni mchango mkubwa sana kwa Umoja wa Mataifa, mpango wa UNSOM na nchi ya Somalia kwa ujumla.

Medali hii maalum ilianzishwa mwaka 1995 kwa kutambua wanajeshi na maafisa wa kiraia wa  polisi wanaohudumu na Umoja wa Mataifa.