Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa nini Anchi za Afrika ya Mashariki zinahofia ongezeko la Madeni:UNECA

Kwa nini Anchi za Afrika ya Mashariki zinahofia ongezeko la Madeni:UNECA

Kiwango cha ongezeko la madeni kimekuwa kikipanda barani Afrika na limbikizo la madeni hayo kwa Afrika Mashariki limeongezeka hata zaidi.

Hayo ni kwa mujibu wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi kwa Afrika UNECA ambayo imesema ni lazima malimbikizo ya madeni yafuatiliwe kwa karibu na kwa uangalifu, kwani madeni sio njia bora ya kufadhili serikali, na badala yake wakusanye rasilimali zingine za ndani .

UNECA inasema nchi ambazo zimefanya vizuri ni zile zilizokusanya mapato ya ndani na huo ndio mtazamo ambao nchi za Afrika zinapaswa kuuchukua.

Andrew Mold ni afisa wa uchumi wa UNECA

(SAUTI YA ANDREW MOLD)

“Kote Afrika kila mwaka ukuaji wa madeni ni asilimia 11 na kwa afrika Mashariki ongezeko ni la haraka zaidi, sasa je mwenendo huu unatish?ni hali ambayo watunga sera wanapaswa kuifuatilia kwa karibu, hususani katika hali ambayo malimbikizo ya madeni yanaongezeka zaidi ya kiwango cha ukuaji wa uchumi”