Malaria haiongozi tena kwa vifo kwa watoto Afrika- WHO

22 Agosti 2016

Malaria sio chanzo kikuu tena cha vifo kwa watoto Afrika Kusini mwa jangwa la sahara, Afrika. Amina Hassan na taarifa kamili..

(TAARIFA YA AMINA)

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, ambalo leo limepitisha azimio jipya lijulikanayo kama "Mfumo wa Malaria Afrika", ambalo lengo lake ni kusaidia nchi wanachama katika kutekeleza vipaumbele maalum ili kutokomeza kabisa malaria Afrika.

WHO inasema ingawa bado safari ni ndefu, visa vya malaria Afrika vimepungua kwa asilimia 66 tangu mwaka 2000. Dr. Frank Lule, mkurugenzi mkuu wa wa kikanda Afrika amesema kilicholeta mafanikio haya Afrika ni..

"Mikakati mitatu ya malaria ni matumizi ya neti zenye dawa, kupulizia dawa ndani ya nyumba, na kudhibiti visa kwa, kuhamishia matibabu mikononi mwa jamii, ambapo kuna uchunguzi wa haraka, ambapo unapanua wigo haraka wa watu kupata matibabu."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter