Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al Mahdi akubali kuhusika na uharibifu wa maeneo ya kidini Timbuktu

Al Mahdi akubali kuhusika na uharibifu wa maeneo ya kidini Timbuktu

Huko The Hague, Uholanzi, kwenye mahakama ya kimataifa ya  uhalifu, ICC, Ahmad Al Faqi Al Mahdi kutoka Mali amekubali makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya maeneo ya kihistoria na kidini huko Timbuktu.

Mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda akisoma mashtaka hayo amedai kuwa Al Mahdi alifanya vitendo hivyo kati ya tarehe 30 Juni 2012 na tarehe 11 Julai 2012, licha ya kuwa yeye ni mwenyeji wa eneo hilo na anafahamu umuhimu wa maeneo hayo kwa jamii ya Mali.

(Sauti ya Bensouda)

“Mashambulizi ya makusudi dhidi ya majengo ya kihistoria na yale yaliyotengwa ya kidini ni kosa kubwa na huleta athari kubwa na kudhoofisha;  kwanza jamii husika lakini pia maeneo ya kijiografia ambako yamejengwa. Ni lazima tuwe thabiti kuazimia kuepusha ukwepaji sheria kwenye uhalifu huu mkubwa.”

Hii ni kesi kwanza ya Mali mbele ya ICC ambapo baadaye wawakilishi wa wahanga wa vitendo hivyo pamoja na upande wa utetezi watatoa taarifa zao.