Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi harusini Uturuki:

Ban alaani shambulio la kigaidi harusini Uturuki:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la kigaidi ,lililofanyika Jumamosi kwenye hafla ya harusi mjini Gaziantep, nchini Uturuki.

Shambulio hilo linalodaiwa kufanywa na mshambuliaji wa kujitolea muhanga , limekatili maisha ya watu 50 na kujeruhi wengine wengi.

Katibu Mkuu ameelezea kusikitishwa kwake na shambulio hilo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo, serikali na watu wote wa Uturuki.

Pia amewatakia nafuu ya haraka majeruhi na kutumai kwamba waliohusika na kitendo hicho cha kikatili watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Amerejea kusisitiza kwamba kuna haja ya kuimarisha juhudi za kikanda na za kimataifa kuzuia na kukabiloiana na ugaidi na ghasia za itikadi kali.