Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la wakimbizi na wahamiaji kutamalaki GA 71

Suala la wakimbizi na wahamiaji kutamalaki GA 71

Suala la wakimbizi na wahamiaji litatamalaki wakati wa kiakao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa cha 71 hapo mwezi Septemba. Nchi wanachama waliafikiana kimsingi kukutana ili kujadili na kupata ufumbuzi wa madhila yanayowakabili wakimbizi zaidi ya milioni 60 kote duniani.

Akizungumzia umuhimu wa kikao maalumu kuhusu wakimbizi na wahamiaji mkurugenzi wa masuala ya baraza kuu na baraza la kiuchumi na kijamii Ion Botnaru amesema Katibu Mkuu Ban Ki-moon and mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM watatia saini makuafa maalumu ambao..

(SAUTI YA BOTNARU)

“Utainua hadhi ya shirika hilo mbele ya Umoja wa Mataifa, na kuimarisha zaidi ushirikiano baiana ya mashirika haya mawili, wana utaalamu na Umoja wa Mataifa una uelewa kwa siasa , hivyo nadhani kufanya kazi kwa karibu pamoja kutasaidia kutoa umuhimu na kulitanabaisha zaidi eneo hili.”

Pia amesema suala la afya halitotupwa mkono

(SAUTI BOTNARU)

“Zika, HIV na ukimwi, malaria, nadhani kikao hicho cha ngazi ya juu cha masuala ya kiafya , chenye mvutu kwa nchi wanachama nadhani watataka kuelezea misimamo yao kuhusu eneo hilo muhimu”

Mada zingine zitakazopewa kipaumbele ni masuala ya wanawake, vijana , mabadiliko ya tabia nchi na malengo ya maendeleo endelevu SDG’s