Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki izingatie wajibu wake wa kimataifa kuhusu haki za binadamu:UM

Uturuki izingatie wajibu wake wa kimataifa kuhusu haki za binadamu:UM

[caption id="attachment_291032" align="alignnone" width="300"]ohapanapaleuturuki

Kundi la wataalamu huru wa umoja wa mataifa wametoa wito kwa serikali ya Uturuki kuzingatia sheria za kimataifa za haki za kibinadamu hata kwa wakati huu ambapo hali ya dharura imetangazwa nchini humo. Wito huo wa wataalamu unakuja wakati ambapo serikali ya uturuki imepuuza jukumu lake la kufuata sheria za kimataifa za haki za kibinadamu baada ya majaribio ya mapinduzi ya mwezi jana, Julai 15 na hususain baada ya kutangazwa kwa hali ya dharura tarehe 20 Julai ambapo raia wengi katika sekta ya Elimu, waandishi wa habari na wanajeshi wamewekwa kizuizini. Zaidi ya hayo kuna madai ya unyanyasaji na hali mbaya kizuizini ambayo inakiuka haki za msingi za kibinadamu