Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Mistura akaribisha kuondolewa wanaohitaji misaada ya matibabu Aleppo.

De Mistura akaribisha kuondolewa wanaohitaji misaada ya matibabu Aleppo.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Bwana, Staffan de Mistura, alitoa ombi maalumu kwa ajili ya kuwahamisha haraka wale wanaohitaji msaada wa matibabu kutoka maeneo yanayozingirwa ya miji ya Fouah na Madaya.

Leo hii de Mistura, amekaribisha habari njema ya kuhamishwa kwa watu hao wanaohitaji matibabu kutoka katika miji hiyo. Watu wapatao 36 wamehamishwa leo na shirika la mwezi mwekundi la mataifa ya Kiarabu SARC, wakiwemo watoto kadhaa na watu wengine wanaohitaji msaada wa matibabu.

Mwakilishi huyo maalumu amewashukuru wote waliofanikisha zoezi hilo, na kusema wakati hii ni hatua njema, maeneo ambayo bado yanazingirwa Wasyria wanahitaji chakula na msaada wa dawa. Amesema maeneo kama Madaya na Fouah,hakuna msafara wowote wa msaada ulioruhusiwa kuingia kwa siku 110 sasa, huku kukiwa na taarifa za kuhitaji haraka msaada wa chakula miji kama Darayya.