Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Honduras nchi hatari kwa watetezi wa haki za binadamu – Wataalam

Honduras nchi hatari kwa watetezi wa haki za binadamu – Wataalam

Honduras imekuwa moja ya nchi zenye uhasama na hatari zaidi kwa watetezi wa haki za binadamu, wameonya leo wataalam wawili wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa na Shirika la Haki la Inter-American, IACHR.

Hadi kufikia sasa karibu watetezi wanane wameuawa nchini huko ambapo watetezi hao wamesema serikali ya Honduras inabidi ichukue hatua zinazofaa kuwalinda watetezi hao ili wafanye kazi zao bila hofu, tishio la vurugu au mauaji.

Michel Forst wa Umoja wa Mataifa na José de Jesús Orozco Henriquez wa IACHR wametoa onyo hilo baada ya mauaji ya kikatili ya Agosti 9, 2016 ya Kevin Ferrera, mwanasheria na kiongozi wa kitengo cha vijana cha chama cha upinzani cha

Liberal.

Wamesema wana wasiwasi kwamba mauaji hayo ya Bwana Ferrera yanahusishwa na kazi yake halali katika ulinzi wa haki za binadamu na hivyo wameomba serikali ichunguze kwa ukamilifu na ufanisi.