Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi langu kwa dunia ni amani, bila kujali ragi, dini wala utokako:Hala Kamil

Ombi langu kwa dunia ni amani, bila kujali ragi, dini wala utokako:Hala Kamil

Tukiwa bado na siku hii, wahenga walinene aisifiaye mvua immenyea au siri ya mtungi aijuaye kata,hayo yamedhirika kwa Bi Hala Kamil na familia yake walioshuhudia kila adha ya vita nchini Syria , wakalazimika kukimbia na sasa wanapata hifadhi nchini Ujerumani. Hadhidi yake inawakilisha mamilioni ya wakimbizi kote duniani. Anasema haelwi ni kwa nini watu wanachagua vita na sio amani kwani alichokishuhudia hatopenda binadamu yoyote kimkute, kwa muktada huo ana ombi..

(SAUTI YA HALA)

“Wito wangu kwa ajili ya amani sio kwa Syria tu. Nataka amani duniani kote bila kujali itikadi wala Imani ya kidini ya mtu, awe muislam au mkristo kwangu si tija.Ninachojali ni kwamba sisi sote ni binadamu.

Naye mkimbizi wa ndani nchini Uganda Sarah Migisa akimshukuru mtu aliyempokea na familia yake baada ya kufurushwa huko Hoima anafunguka

(SAUTI YA SARAH)