Skip to main content

UM una kila kitu unachohitaji kuwasaidia masikini:O’Brien

UM una kila kitu unachohitaji kuwasaidia masikini:O’Brien

Tuannze na madhila yanayoighubika dunia. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu inaelezwa kuwa watu Milioni 130, idadi ambayo ni kubwa zaidi kufikiwa, hivi sasa wanaishi kwa kutegemea misaada ya kibinadamu. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats

Katika kuadhimisha siku hii video maalum imeandaliwa ikionyesha madhila yanayokumba watu hao walioenea kuanzia Afrika, Asia, Amerika hadi Ulaya.

Nats..

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake ametaka viongozi watimize ahadi ya kumaliza mizozo na wakumbuke kuwa kila mtu anawajibika kwa utu wa mwenzake.

Naye mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa mataifa Stephen O'Brien, akizungumzia siku hii amesema..

(SAUTI YA O'BRIEN)

 "Ni siku ambayo sote tunapaswa kuwa msitari wa mbele na kuchukua hatua, lakini pia kutafakari fursa kama raia wa kimataifa , kuchagia vilivyo katika kukidhi mahitaji wa binadamu wenzetu duniani ambao wako katika hali mbaya"

 Ameongeza rasilimali ipo, watu wapo na nia ipo sasa kinachohitajika ni..

(SAUTI YA O'BRIEN 2)

“Tunahitaji kushirikiana vizuri kwa pamoja ili kuhakikisha tunazitumia rasilimali hizo ipasavyo, zaidi ya hayo ni kuhakikisha tunayo fursa salama bila vikwazo, tunaidai kama haki, masula ya kibinadamu kama zisemavyo sheria za kimataifa ni lazima yapewe fursa isiyo na pingamizi kwa mahitaji yoyote yatanayojitokeza na vyovyote yanavyotokea".