Skip to main content

Zaidi ya watu 850 wauawa nchini Ufilipino kufuatia msako wa wahalifu

Zaidi ya watu 850 wauawa nchini Ufilipino kufuatia msako wa wahalifu

Ufilipino ni lazima ikomeshe mauaji ya kinyume cha sheria dhidi ya watu wanaoshukiwa kwa makosa yanayohusiana na mihadarati. Wito huo umetolewa na wataalamu huru wawili wa Umoja wa Mataifa.

Watu zaidi ya 850 wameripotiwa kuuawa kati ya mwezi Mai na Agosti wakati Duterte alipochaguliwa kuwa Rais na kuahidi kupambana na uhalifu. Na zaidi ya 650 kati ya hao wameuawa katika wiki sita zilizopita pekee.  Madai ya biashara haramu ya dawa za kulevya ni lazima yashughulikiwe mahakamani, na sio kwa mtutu wa bunduki mitaani wameongeza wataalamu hao.

Wameitaka serikali ya nchi hiyo kuchukua mara moja hatua za lazima kuwalinda watu wote dhidi ya mauaji ya kulengwa na ya kinyume cha sheria, wakisisitiza kwamba Ufilipino ina wajibu wa kisheria kuhakikisha haki ya kuishi kwa kila raia wake bila kujali anashukiwa kwa uhalifu ama la.