Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka pande hasimu Sudan kujadili kusitisha uhasama

Ban azitaka pande hasimu Sudan kujadili kusitisha uhasama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa na pande hasimu nchini Sudan kushindwa kufikia muafaka wa usitishaji mapigano kwenye majimbo ya Darfur, Blue Nile na Kordofan Kusini. Rosemary Musumba na taarifa zaidi...

(TAARIFA YA ROSE)

Pande hizo zilikutana mjini Addis Ababa kuanzia Agost 5 hadi 14 mwaka huu na Katibu Mkuu amezitaka kuanza tena majadiliano, kuzingatia mchakato wa amani walioafikiana na kujizuia na majaribio yoyote ya kuzidisha ghasia Dafur na kwenye majimbo hayo mengine mawili.

Ban amersisitiza kwamba hakutakuwa na suluhu yoyote ya kudumu ya amani .endapo uhasama utaendelea.

Pia ameshukuru juhudi za Muungano wa Afrika, mpango wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa na muungano wa Afrika Darfur UNAMID na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sudan na Sudan Kusini kutaka kuleta amani ya kudumu nchini Sudan.