Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikutano haina maana kama misaada haifiki Syria- de Mistura

Mikutano haina maana kama misaada haifiki Syria- de Mistura

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura amelazimika kuahirisha kikao cha kikosi kazi cha kimataifa kuhusu usaidizi wa kibinadamu nchini humo akisema kwamba hakina maana kufanyika ikiwa misaada ya kibinadamu haiwafikii walengwa.

Akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Uswisi hii leo baada ya kuahirisha kikao hicho kilichofanyika kwa dakika Nane, akisema kinachoonekana ni kipaumbele Syria ni mapigano huku watu wenye mahitaji wakiendelea kuhaha, hivyo ..

 (Sauti ya de Mistura)

“ Ndio maana leo nimeamua kuahirisha haraka kikao cha kikosi kazi kwa sababu tunachotaka leo ni hatua. Ujumbe wetu ni dhahiri tunataka angalau sitisho la mapigano kwa saa 48 ili misafara ya kibinadamu iweze kwenda bila vikwazo vyovyote hadi Aleppo kwa sababu mji ni mmoja, mashariki na magharibi.”