Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na serikali ya Uganda wahaha kudhibiti kipindupindu wilayani Adjumani

UNHCR na serikali ya Uganda wahaha kudhibiti kipindupindu wilayani Adjumani

Serikali ya Uganda na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) wanachukua hatua za kudhibiti mlipuko wa kipindupindu, kwenye makazi mapya ya wakimbizi ya Pagirinya wilayani Adjumani. Brian Lehander na habari zaidi..

(TAARIFA YA BRIAN)

Wakimbizi 49 wa Sudan Kusini na raia mmoja wa Uganda wamethibitika kuambukizwa kipindupindu , na 44 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa wakati wagonjwa wawili wakisalia kwenye karantini.

Hatua zaidi zimechukuliwa na serikali ya Uganda na UNHCR kuzuia maradhi hayo kusambaa zaidi. Miongoni mwa hatua hizo ni kusafisha kwa dawa maalumu nyumba za watu walioambukizwa pamoja na mifumo yao ya maji, huku kampeni ya ullimishaji ikifanyika nyumba kwa nyumba.

Pia uuzaji wa vyakula mitaani umedhibitiwa sanjari na kusafisha maji kwa tembe za chlorine, kusafisha mapipa ya takataka na kunawa mikono kwa sabuni . Makazi ya Pagirinya yanahifadhi zaidi ya wakimbizi 30, 000 wa Sudan Kusini waliowasili wiki sita zilizopita.