Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magugu maji tishio kwa uvuvi Uganda

Magugu maji tishio kwa uvuvi Uganda

Nchini Uganda uwepo wa magugu maji ni tishio kwa uvuvi ziwani Albert na hivyo hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa kwani uwepo wa magugu hayo unakwamisha shughuli za kijamii na kiuchumi ikiwemo uvuvi.

Wavuvi wanahaha hawajui la kufanya kama anavyosimulia mwandishi wetu John Kibego aliyekwenda Ziwa Albert kushuhudia kilio cha wavuvi na kukutana na wadau hao wa uvuvi.