Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 taka za sumu zimwagwe nchini Cote D'Ivoire, wahanga hawajaridishwa

Miaka 10 taka za sumu zimwagwe nchini Cote D'Ivoire, wahanga hawajaridishwa

Kuelekea kumbukumbu ya miaka 10 tangu kumwagwa kwa taka za sumu nchini Cote D'Ivoire, kikundi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa kimeiomba serikali ya nchi hiyo, jumuiya ya mataifa na wote wanaohusika kutumia fursa ya siku hiyo kushughulikia suala la haki za binadamu litokanalo na kisa hicho.

Wataalam hao pia wameitaka kampuni ya Trafigura inayohusika na kisa hicho kiitwacho Probo Koala ambayo ni meli iliyokuwa imebeba shehena ya taka hizo za sumu, itoe habari zote juu ya taka hizo za sumu na na madhara yoyote ya kiafya na kimazingira yanayohusishwa nazo.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa takribani watu 15 walifariki dunia, 69 walilazwa hospitalini na wengine zaidi ya mia moja na nane elfu walihitaji matibabu

Hadi sasa wahanga wa taka hizo hawajafahamu hatma ya afya zao wakisema kuwa hawajaweza kumudu matibabu tangu matibabu ya bure baada ya Oktoba 2006.

Halikadhalika wanalalama juu ya vichwa kuuma magonjwa ya ngozi, matatizo kupumua na hata harufu itokayo eneo husika pindi mvua ikinyesha.

Wamiliki wa taka hizo walikuwa kampuni ya Uingereza na Uholanzi ambapo tarehe 109 Agosti walizimwaga mjini Abidjan na katika vituo vingine ambavyo havijajulikana hadi leo.

Kampuni ya Trafigura ilishindwa kumwaga taka hizo uholanzi kwa kuwa gharama yake ilikuwa juu.