Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani mauaji huko DRC

Baraza la usalama lalaani mauaji huko DRC

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameshutumu vikali mauaji ya takriban raia hamsini yaliotokea kwenye kijiji cha Rwaonga jimbo la Kivu Kaskazini, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mauaji yanayodaiaw kufanywa na kundi la waasi wa ADF.

Katika taarifa yao, wajumbe hao wameonyesha wasiwasi wao juu ya vurugu zinazoendelea kwenye jimbo hilo na wameitaka serikali ya DRC kuchukua hatua za haraka na uchunguzi kulingana na sheria za kimataifa ili kukabiliana na tishio linazosababishwa na makundi yaliyojihami katika sehemu hiyo.

Wajumbe hao pia pia wamesisitiza msaada wao  kwa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO na kutaka pande zote husika kufanya kazi kwa pamoja na ujumbe huo utimize lengo lake nchini DRC