Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 71 cha baraza kuu kitakuwa muhimu sana:Botnaru

Kikao cha 71 cha baraza kuu kitakuwa muhimu sana:Botnaru

Kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachotarajiwa kuanza mwezi ujao wa Septemba kitakuwa muhimu sana.

Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya baraza kuu na baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa Ion Botnaru.

Akizungumza na Umoja wa Mataifa amesema kikao hicho ni mwanzo wa muongo mwingine katika maisha ya Umoja wa Mataifa ambayo kwa sasa yanakabiliwa na changamoto nyingi, lakini akasema wana wanatajajia mengi mwaka huu..

(SAUTI BOTNARU)

“Tunatarajia mjadala wa baraza kuu mwaka huu ambapo wakuu wa nchi na serikali watakuja na mitazamo yao ya jinsi ya kutatua changamoto zote ambazo zinaikabili jumuiya ya kimataifa iwe ni hali ya mashariki ya kati au suluhu ya migogoro Afrika.”

Akagusia pia mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa na kibarua kinachumsubiri baada ya kupata mapendekezo kadhaa kutoka kwa wagombea wote 12..

(SAUTI YA BOTNARU)

"Bila shaka Katibu Mkuu ajaye, mwaume au mwanamke itabidi azingatie mawazo yote yaliyotolewa ili kuwa na Umoja wa Mataifa wenye ufanisi zaidi na kuboresha utendaji kuufanya Umoja wa Mataifa kwenda sanjari na karne ya 21".