Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani katika hatihati ya janga baya la asili tangu Sandy:UNISDR

Marekani katika hatihati ya janga baya la asili tangu Sandy:UNISDR

Jimbo la Louisiana nchini Marekani liko katika hatihati ya kile kinachoonekana kama kukumbwa na janga baya zaidi la mafuriko nchini Marekani tangu wakati wa kimbunga Sandy , miaka mine iliyopita, na hivyo kuhidhirisha umuhimu wa jukumu la kupunguza hatari ya majanga kabla hayajatokea.

Hayo ni kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR. Jumapili wiki hii Rais Barack Obama ametangaza janga kubwa la mafuriko jimboni Louisiana ikiwemo katika parishi zilizoathirika sana za Tangipahoa, St. Helena, Baton Rouge Mashariki na Livingston.

Orodha hiyo inatarajiwa kuongezeka, wakati lazima ya watu kuhama ikiendelea kwenye mji wa Lake Arthur.

Zaidi ya zskari wa ulinzi wa taifa 1,700 wamekusanywa jimboni humo na wengine wanaelekea kwenye maeneo yaliyoathirika. Watu 20,000 wameokolewa kwenye maeneo yaliyofurika Kusini mwa Louisiana, na idadi ya waliopoteza maisha imefikia saba, huku maeneo ya jirani ya Mississippi yameathirika pia.

UNISDR imesisitiza kuwa maandalizi ya kupunguza majanga yanaokoa maisha na ni kauli mbiu itakayogonga vichwa vya habari mnamo Oktoba 13 kwenye siku ya kimataifa ya upunguzaji hatari ya majanga.