Skip to main content

Zambia yapongezwa kwa uchaguzi wa amani na utulivu:UM

Zambia yapongezwa kwa uchaguzi wa amani na utulivu:UM

Umoja wa Mataifa umeipongeza serikali ya Zambia na watu wake kwa kufanya uchaguzi mkuu kwa amani na mpangilio. Brian Lehander na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA BRIAN)

Uchaguzi huo wa Rais, wabunge serikali za mitaa na kura ya maoni ya kuhusu mswada wa haki umefanyika Agost 11.

Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Ban Ki-moon akikumbuka ule alioushuhudia  alipozuru nchi hiyo mwaka 2012 amesema, Zambia ina historia ya uchaguzi wa amani na demokrasia na kwa muktada huo anazikumbusha pande zote na hususani viongozi wa kisiasa na wafuasi wao, kwamba wanajukumu la kukana machafuko na kujizuia kutumia lugha za chuki na uchochezi.

Pia amewaasa kutatua tofauti zao au migogoro yoyote ya uchaguzi kupitia sheria za kikatiba zinazoenda sanjari na viwango vya kimataifa. Na kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Zambia katika masuala ya demokrasia na maendeleo endelevu.