Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na WHO walaani shambulio dhidi ya hosptiali ya MSF Yemen

Ban na WHO walaani shambulio dhidi ya hosptiali ya MSF Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelani shambulizi dhidi ya hospitali iliyoko eneo la Haijjah, nchini Yemen, hospitali inayomilikiwa na madaktari wasio na mipaka, MSF.

Amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za kibinadamu za kimataifa huku shirika la afya duniani WHO likilaani shambulio hilo lililosababisha vifo vya watu 11 wakiwemo wafanyakazi wa MSF.

Wakati wa shambuli hilo kulikuwepo na wagonjwa 25 wakifanyiwa upasuaji na watoto wachanga 13.

Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO.

(Sauti ya Tarik)

‘‘WHO kwa mara nyingine inazitaka pande zote kuzingatia wajibu wao chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu kulinda wahudumu wa afya na vifaa tiba. Tangu kukuwa  kwa mgogoro  mwezi Machi mwaka jana, zaidi ya wahudumu wa afya 13 wamefariki na 23 kujeruhiwa.’