Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMI yalaani mauaji ya mwanahabari wa kikurdi

UNAMI yalaani mauaji ya mwanahabari wa kikurdi

Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Gyorgy Busztin, ameilaani vikali muaji ya mwanahabari yaliyotokea kwenye mji wa Dohuk jimbo la Kurdistan nchini Iraq.

Mwanahabari huyo wa kujitegemea Widah Hussein alitekwa nyara mnamo Jumamosi ya tarehe 13 mwezi huu wa Agosti na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami na baadaye alipatikana pembeni mwa barabara akiwa amejeruhiwa na alifariki dunia wakati akipata matibabu hospitalini.

Katika taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, Bwana Busztin pamoja na kulaani ameiomba serikali ya eneo hilo la Kurdistan kuhakikisha usalama na ulinzi wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari.

Nimesikitishwa sana na mauaji ya mwana habari huyu, tabia kama hii inaonyeshakukua kwa vitisho vinavyoelekezwa kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kati eneo hii la Kurdistan nchini Iraq, amesema Bwana Busztin, huku akisema kuwa matukio kama hayo yanatishia uhuru wa kujieleza na kupata habari ambao ni muhimu sana katika demokrasia ya nchi.

Mwili wa Ali ulikutwa na majeraha kote mwilini na zaidi ya hayo alikuwa amejeruhiwa pia kichwani ambapo inaonyesha alipigwa na kuteswa alipokuwa matekani.

Tayari uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo cha kifo chake.