Skip to main content

Said Djinnit amelaani vikali mashambulizi dhidi ya raia Beni DRC

Said Djinnit amelaani vikali mashambulizi dhidi ya raia Beni DRC

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa eneo la maziwa makuu Said Djinnit, amelaani vikali mauaji ya watu 36 wakiwemo wanawake kwenye mji wa Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Shambulio hilo linalosadikiwa kufanywa na kundi la ADF lilifanyika katika kitongoji cha Rwangoma, karibu na mji wa Beni Agost 13 hadi 14. ADF ni kikundi cha waasi wenye asili ya Uganda na kinaendesha operesheni zake Mashariki mwa DRC.

Djinit ambaye ametumba salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa DRC, amerejea msimamo wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA DJINIT)

“Tumetoa tamko kuunga mkono matamko mengine kulaani vikali , lakini pia kuvikana vitendo hivyo vya kigaidi, kwa sababi jinsi vinavyotekelezwa vinashabihiana na njia zinazotumiwa na magaidi, kushambulia raia wasio na hatia kweny ni kitendo kisichokubalika”

Ameongeza kuwa shambulio halitozima nia ya pamoja kuvisambaratisha vikundi vya waasi ambavyo vinaendelea kusababisha simanzi na mauaji Mashariki mwa DRC.