Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yawainua vijana Katanga DRC kwa miradi mbalimbali ya maendeleo

ILO yawainua vijana Katanga DRC kwa miradi mbalimbali ya maendeleo

Shirika la Kazi Duniani(ILO) limeanzisha mpango maalumu wa mafunzo na ujasiria mali mjini Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Lengo ni kuwawezesha vijana kujitegemea kwa kuanzisha miradi mbalimbali kukabiliana na changamoto ya ajira.

Mradi huo unaofahamika kama PAEJK unajumuisha ufugaji wa kuku, uhunzi, umakenika, komputa na kilimo cha bustani za mboga na matunda. Kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.