Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio kwenye shule mjini Sa’ada Yemen lalaaniwa na UM

Shambulio kwenye shule mjini Sa’ada Yemen lalaaniwa na UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulizi lilnalosemekana kuwa ni la anga dhidi ya shule kwenye jimbo la Sa'ada Kaskazini mwa Yemen tarehe 13 Agosti.

Katibu Mkuu amesikitishwa kwamba raia wakiwemo watoto ndio wanaobeba gharama za mapigano na operesheni za kijeshi nchini Yemen.

Ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa vitendo hivyo vya kikatili na kuzitaka pande zote katika mzozo kuchukua hatua za lazima kuzuia ukiukaji zaidi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu , na kufanya kila liwezekanalo kwa mamlaka waliyonayo kuwalinda raia na miundombinu ya raia hao.

( SAUTI FARHAN)

"Katibu Mkuu amesisitiza suluhu ya kijeshi kwa mgogoro wa Yemen, na ametoa wito kwa pande hasimu kuongeza muda bila kuchelewa na kwa nia njema mhusiano na mwakilishi wake maalumu Yemen kwa lengo la kusaka suluhu."