Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wanawake ni muhimu katika amani-UNMISS

Mchango wa wanawake ni muhimu katika amani-UNMISS

Kitengo cha Masuala ya Jinsia cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini(UNMISS) kimehutubia wanawake kuhusu azimio la Baraza la Usalama nambari 1325, linalohimiza serikali na wadau wengine kuongeza ushiriki wa wanawake na mtazamo wa jinsia katika juhudi za  amani na usalama.Taarifa ya Brian Lehander inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Brian)

Afisa wa masuala ya jinsia wa UNMISS Mihad Abdallhah amekutana na wanawake katika eneo la Nhialdu kata ya Rubkona, na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa mchango wao katika kukuza amani na usalama wa jamii zao, akisema "Wanawake hawapaswi kupuuzwa wakati wa kufanya maamuzi katika familia, jamii na  ngazi ya juu na katika nyanja zote za maisha, ameongeza  kuwa wanawake hubeba mzigo mkubwa wa maafa yaletwayo na migogoro na vita.

Miongoni mwa mambo mengine yaliyojitokeza ,wanawake hao wameomba wadau wa masuala ya kibinaadamu kuwasaidia na msaada usio wa chakula kama vyandarua na betrii za tochi.