Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcheza piano nguli Zade Diran kuwa balozi mwema wa UNICEF

Mcheza piano nguli Zade Diran kuwa balozi mwema wa UNICEF

Mtunzi na mcheza piano mashuhuri Zade Dirani kutoka nchini Jordan Leo ameteuliwa na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuwa balozi wake mwema wa kikanda

Dirani atawakilisha kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini , kwa kujikita zaidi katika kwa watoto wasiojiweza hususani waliokumbwa na vita, ghasia na umasikini.

Akimkaribisha rasmi , naibu mwakilishi wa UNICEF Jordan Bi Ettie Higgins amesema mabalozi wema

(SAUTI HIGGINS)

“Ni mionongoni mwa sauti imara zinazoleta mabadiliko kitaifa na kimataifa kuboresha maisha ya watoto na vijana , na UNICEF inathamini sana mchango wao wa kuleta mabadiliko mazuri kwa watoto, na tunafurahi kuwa nawe kama miongoni mwao , na pia mmoja wetu”

Diran ameshatumbuiza kwa mwaliko maalumu mbele ya watu wengi mashuhuri duniani ikiwemo familia ya kifalme ya Jordan, Malkia Elizabeth wa Uingereza, Dalai Lama na hayati Nelson Mandela.