Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku tatu za maombolezo DRC kufuatia mauaji ya raia Beni

Siku tatu za maombolezo DRC kufuatia mauaji ya raia Beni

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo ni siku ya pili ya maombolezo ya kitaifa kufuatia mauaji ya raia 36 yaliyotokea kwenye kijiji cha Rwangoma, huko Beni jimbo la Kivu Kaskazini usiku wa Jumamosi kuamkia jumapili.

Serikali ya DRC ilitangaza maombolezo hayo ya kitaifa bendera zikipepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia Jumapili ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Maman Sambo Sidikou ametuma salamu za rambirambi huku akilaani kitendo hicho cha waasi wa ADF alichoita ni ukatili dhidi ya raia.

Bwana Sidikou ambaye ni pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO amesisitiza azma ya umoja huo kuendelea kusaidia harakati za jeshi la serikali, FARDC na polisi wa kitaifa za kulinda raia.