Vijana wajadili jinsi ya kushiriki kufanikisha SDGs

Vijana wajadili jinsi ya kushiriki kufanikisha SDGs

Wiki hii, kuanzia tarehe 10 hadi 12 Agosti, ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Vijana, vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekusanyika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye jukwaa linalowezesha mazungumzo na kuibua ubia baina ya vijana wenye umahiri mkubwa, maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.

Baraza hilo la vijana lilimulika hasa jinsi ya kuwezesha vijana walio uongozini na vijana waliobobea katika taaluma mbali mbali, ili washiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 kuhusu maendeleo endelevu. Kwa mengi zaidi kuhusu Baraza hilo la vijana, ungana na Joshua Mmali katika makala ifuatayo.