Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Thailand ya Alhamisi na Ijumaa

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Thailand ya Alhamisi na Ijumaa

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa Thailand Alhamisi na Ijumaa.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulizi hayo na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Pia ametoa pole kwa serikali na watu wa Thailand kufuatia zahma hiyo na kusema anatumai waliohusika na uhalifu huo watafikishwa kwenye mkono wa sheria haraka iwezekanavyo.

Duru zinasema watu wanne wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi hayo huku wengine wengi wakijeruhiwa .