Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je ni usikivu au umakinifu ?

Je ni usikivu au umakinifu ?

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “usikivu” na “umakinifu”  ambapo mchambuzi wetu Nuhu Zuberi Bakari, Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema ni maneno mawili yanayotumiwa kama yanafanana lakini hayafanani. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii amesema neno usikivu linatokana na kusikiliza kwa masikio na umakinifu ni kuwa makini kwa kufuatilia hata kama kitendo hakisemwi bali kinatazamwa. Bwana Nuhu anasema mtu anaweza kuwa makini lakini hasikii kinachosemwa au akawa anasikiliza lakini si makini. Hebu fuatilia kwa makini katika taarifa hii.