Mchanganyiko wa zahma zinazoikabili dunia hivi sasa ni changamoto kwa vijana:Ban
Kuzuka kwa vitisho, ghasia za itikadi kali, mabadiliko ya kisiasa, kuyumba kwa uchumi na mabadiliko ya kijamii , kwa pamoja ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili vijana kote duniani. Assumpta Massoi na taarifa kamili.
(Taarifa ya Assumpta)
Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya vijana, akisisitiza kwamba hakuna anayejua zaidi changamoto zilizopo na njia bora za kuzikabili kama vijana wenyewe. Ndio maana anawataka vijana kupaza sauti zao na viongozi kusikiliza
(SAUTI YA BAN)
“Ni muda wa kujitoa kwa ajili ya vijana na kufanya kazi kwa pamoja na vijana, na ujumbe wangu kwa vijana ni kwamba mna uwezo, kuifanya dunia yetu kuwa bora na kwa viongozi nasema wasaidieni vijana kutumia nguvu hii kwa faida yetu wote, katika siku ya kimataifa ya vijana nasimama na ulimwengu wa vijana kuongoza leo kwa ajili ya mustakhbali bora wa kesho.”
Naye mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya vijana Ahmad Al-Hendawi akiwalenga vijana wa Libya katika wakati huu wa machafuko na kusema atapigia chepuo ushirikishwaji wao katika mchakato wa amani, lakini akawaasa vijana kutokata tamaa, na wajikite katika kujenga mustakhbali bora wa taifa lao