Skip to main content

Rwanda yaahidi kusimama na watu wa Sudan Kusini katika masuala ya amani

Rwanda yaahidi kusimama na watu wa Sudan Kusini katika masuala ya amani

Rwanda imesema imejidhatiti kushikamana na watu wa Sudan Kusini katika nia yao ya kusaka amani ya kudumu.

Hakikisho hilo limetolewa wakati wa gwaride maalumu la kuwatunukunia medali wanaanga 165 wa Rwanda wanaofanya kazi na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS.

Kikosi hicho cha wana anga kinachojumuisha wanawake 10 wakiwemo kama marubani, wahandisi na maafisa mipango, kimetunukiwa kwa kutoa huduma za usafiri kwa niaba ya UNMISS katika miezi 11 iliyopita.T

Akizungumza wakati wa hafla hiyo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNMISS Ellen Margrethe Loej amesema kikosi hicho cha Rwanda kimekuwa bega kwa began a watu wa Sudan Kusini

(SAUTI YA LOEJ)

“ Kikosi hiki kimekuwa na jukumu muhimu la kuwawezesha wanajeshi kusafiri, kufanya upepelezi, na ndege za doria kutoa usafiri kwa ajili ya matibabu kusaidia safari za mipango. Kimefanikiwa pia katika operesheni za uokozi za wafanyakazi wa UNMISS na watoto waliotekwa Ethiopia.”

Naye kamanda wa kikosi Brigedia jenerali Andrew Kagame amesisitiza azma ya taifa lake kwa amani ya Sudan Kusini

(SAUTI YA ANDREW KAGAME)

“Ni kwa muktada huu ndio serikali ya Rwanda ikatumia vikosi viwili vya ardhini na hiko cha anga kilichotunukiwa leo. Kwa helkopta zake za kijeshi , kikosi hiki kimeweza kufanya kazi kwenye maeneo yenye hatari kubwa”