Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP inafurahi kusaidia vita dhidi ya ufisadi Iraq:

UNDP inafurahi kusaidia vita dhidi ya ufisadi Iraq:

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na serikali ya Iraq leo wametia saini makubaliano mjini Baghdad ya kusaidia kuimarisha uwezo wa serikali ya nchi hiyo , kubaini, kuchunguza na kuchukulia sheria kesi za ngazi ya juu za ufisadi.

Naibu mkuu wa watumishi kutoka ofisi ya waziri mkuu ,Naoufel Al-Hasan, amesema kukomesha ukwepaji sheria ni kitovu cha agenda ya mabadiliko yao.

Akiongeza kuwa wameimba UNDP kutoa msaada wa kiufundi ili kuimarisha uwezo wa serikali katika kuchunguza kesi za ufisadi na kuzichukulia hatua.

Naye mwakilishi mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UNDP nchini Iraq Bi. Lise Grande, amesema UNDP iko tayari kusaidia mchakato wa mabadiliko kwa njia yoyote watakayoweza.Amesema siku zote mabadiliko ni magumu nan yeti, lakini karibu wanalishinda kundi la Daesh, hivyo kuimarisha uwezo wa serikali ni kipaumbele.