Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saa tatu kusitisha mapigano Aleppo hazitoshi- de Misturra

Saa tatu kusitisha mapigano Aleppo hazitoshi- de Misturra

Mapigano yakizidi kushika kasi huko Aleppo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura amesema muda wa saa tatu uliopendekezwa na Urusi wa kusitisha mapigano ili kuwezesha ufikishaji misaada ya kibinadamu, hautoshi. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Ripoti za pendekezo hilo la Urusi zilipazwa na vyombo vya habari siku ya Jumatano ambapo hii leo akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Uswisi Bwana de Mistura amesema ni jambo ambalo wamejadili katika kikao cha kikosi kazi cha kimataifa kuhusu usaidizi wa kibinadamu nchini Syria.

(Sauti ya de Mistura)

“Kwanza kabisa sisi Umoja wa Mataifa hatukuhusishwa. Pili kutokana na kile tunachosikia kutoka kwa mratibu wetu Yacoub El Hilo aliyeko Damascus, saa tatu hazitoshi. Tumekuwa tunasisitiza tunahitaji saa 48.”

Hata hivyo amesema..

(Sauti ya de Mistura)

“Tumebaini leo kutoka shirikisho la Urusi fursa na utayari wa kujadili haraka iwezekanavyo na Umoja wa Mataifa jinsi ya kuboresha kile ambacho kwa mtazamo wetu tumeona ni wazo la awali ambalo hatukishirikishwa,  lakini mratibu wetu wa kibinadamu Damascus ameona halitoshelezi.”