Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwafunga wahamiaji ni kukiuka haki za binadamu-Zeid

Kuwafunga wahamiaji ni kukiuka haki za binadamu-Zeid

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anawasiwasi mkubwa na tabia ya kutojali haki za binaadamu inazotekelezwa na Bulgaria dhidi ya wahamiaji. Amesema leo kwamba ofisi yake imebaini sera zinazowakandamiza wahamiaji walipotembelea nchi hiyo miezi minane iliyopita.

Zeid amesema wahamiaji ni watu walio katika hali ngumu na wanahitaji kulindwa sio kunyanyaswa. Ravina Shamdasani ni msemaji wa Ofisi hiyo..

(Ravina Cut 1)

"Kuwashitaki na kosa la jinai na kuwafunga wanapoingia na wapotaka nje ya nchi inawaweka katika hali mbaya na kuwaweka katika mtazamo ambapo huruhusiwi kuingia nchini na huruhusiwi kutoka bila ya kufungwa jela"

Kamishna Mkuu ametoa wito kwa serikali ya Bulgaria kupambana na wananchi wanaochukua sheria mikononi na kuweka sera zitakazo walinda wahamiaji, na amesema chuki dhidi ya wageni na waislamu ni tishio lenye kuitia wasiwasi mkubwa Ulaya na serikali ya Bulgaria haichukui hatua za kutosha kupambana na mwenendo huu wa kutisha.