Mashirika ya UM yalaani shambulio la kigaidi hospital Pakistan

10 Agosti 2016

[caption id="attachment_291635" align="alignleft" width="350"]hapanapaleunesco

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamepaza sauti zao pia kulaani vikali shambulio la kigaidi kwenye hospital nchini Pakistan mapema wiki hii.

Zaidi ya watu 70 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga mjini Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan alipojilipua kwa bomu Jumatatu.

Wengi wa waliopoteza maisha ni mawakili walikuwa hospitalini hapoi kuomboleza kifo cha Rais wa baraza la wanasheria ambaye aliaga dunia baada ya kupigwa risasi mapema siku hiyo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limelaani vikali shambulio hilo na kusema suala la afya ni lazima liheshimiwe wakati wote.

Waandishi wawili wa habari waliokuwa wakiripoti wakati wa shambulio nao pia wamepoteza maisha , kwa mujibu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNESCO, vifo vya waandishi hao katika shambulio la kikatili namna hiyo ni kuandamiza uqwezo wa wananchi kupata taarifa kitu ambacho ni pigo kwa uongozi bora na demokrasia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud