Hali ya usalama Kivu Kaskazini bado tete- MONUSCO
Kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO unasema hali ya usalama kwenye jimbo la Kivu Kaskazini inasalia kuwa tete na haitabiriki kutokana na vitendo vinavyofanywa na vikundi vilivyojihami katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.
Kaimu msemaji wa jeshi la MONUSCO, Yassine Kasmi ametaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na mashambulizi, uporaji, mauaji, ukatili wa kingono na utozaji kodi kinyume cha sheria.
Amesema mapigano baina ya vikundi hivyo vilivyojihami yamesababisha siyo tu vifo miongoni mwao bali pia raia kukimbia makazi yao na kwamba,…
(Sauti ya Yassine)
“Katika eneo la Beni, vikosi vya serikali, FARDC kwa usaidizi wa jeshi la MONUSCO wanaendeleza operesheni iitwayo Usalama kwa lengo la kuweka shinikizo la kijeshi dhidi ya waasi wa ADF.”
Amezungumzia pia harakati za kuimarisha usaidizi kwa binadamu jimboni Kivu Kaskazini akitaja ukarabati wa daraja kwenye eneo la Rwindi, Mashariki mwa Buleusa uliofanywa na MONUSCO na hivyo amesema..
(Sauti ya Yassine)
“Ni muhimu sasa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa kuharakakisha upelekaji wa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula kwenye mji wa Beleusa.”