Matangazo yanayowalenga watoto yadhibitiswe:Wataalam UM

10 Agosti 2016

Katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana hapo Ijumaa Agosti 12, wataalamu wawili wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu, wameonya kuhusu athari za matangazo ya biashara yanayowalenga watoto wadogo.

Wataalamu hao huru, Juan Pablo Bohoslavsky, anayehusika na madeni ya nje na haki za binadamu na mwakilishi maalumu kuhusu haki ya afya Dainius Püras, wamesema matangazo hayo ni yale yanayowajengea watoto utamaduni wa matumizi ya kupindukia na hulka ya madeni, na wamezitaka serikali kote duniani kudhibiti matangazo yanayowalenga watoto moja kwa moja.

Wamesema ujumbe wa biashara una uwezo wa kujenga tabia ya watoto ya muda mrefu katika muktada wa matumizi na masuala ya fedha.

Wameongeza kuwa pia matangazo hayo yanaweza kusababisha tabia isiyo bora kwa watoto wangali wadogo na akuathiri maisha yao ya baadaye, hasa katika kununu vitu ambavyo si vya lazima bila kujali athari za muda mrefu za kifedha na kiafya, kama vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukali au mafuta.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter