Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kusainiwa kwa makubaliano ya kumaliza migogoro Sudan

Ban akaribisha kusainiwa kwa makubaliano ya kumaliza migogoro Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha makubaliano ya mkakati wa kumaliza migogoro nchini Sudan baina ya vikundi vya upinzani nchini humo, mnamo Agosti Nane, 2016.

Maafikiano hayo yalipendekezwa na jopo la utekelezaji la ngazi ya juu la Muungano wa Afrika (AU), na yalitiwa saini na serikali ya Sudan mnamo Machi 21, 2016.

Taarifa ya msemaji wake imesema Ban ametiwa moyo na hatua hiyo muhimu ya kuelekea kumaliza vita na migogoro nchini Sudan.

Aidha, Ban ametoa wito kwa pande zote Sudan kuendeleza kasi ya nzuri na kuendeleza juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha uhasama, kuwezesha wahudumu wa kibinadamu kufikia maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, na mchakato wa kufikia makubaliano ya kina kupitia mazungumzo jumuishi ya kitaifa.