Skip to main content

Serikali zahimizwa kupitisha mkataba mpya kuhusu wakimbizi na wahamiaji

Serikali zahimizwa kupitisha mkataba mpya kuhusu wakimbizi na wahamiaji

Serikali zinapaswa kuunga mkono mkataba mpya kuhusu wakimbizi na wahamiaji, ili ziweze kuchukua hatua zaidi kulishughulikia tatizo la wakimbizi.

Hayo ni kwa mujibu wa Karen AbuZayd, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano kuhusu jinsi ya kushughulikia idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji, ambao utafanyika mnamo Septemba 19, 2016, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.

Rasimu ya mkataba mpya kuhusu wakimbizi na wahamiaji imeafikiwa wiki hii na wawakilishi wa nchi wanachama 193, na itakuwa msingi wa mkutano huo wa Septemba wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji.

Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa, Bi Abu Zayd ameeleza kwa muhtasari kuhusu rasimu hiyo..

(Sauti ya Karen Abu Zayd)

“Nadhani tulichoafikia ni ufanisi mkubwa sana. Na rasimu tuliyoibuka nayo inatoa vitu vingi, na ahadi zote zilizowekwa mle zimetumia maneno mazito mazito. Nchi wanachama kwa ujumla, na kwa kukubaliana, zinadhamiria kuchukua hatua; zinawajibika, na zinasema kuwa zinaenda kuchukua hatua, na nyingi zinadhamiria kufanya hivyo. Lakini kwa ujumla, zimekubaliana kuhusu vitu vingi vipya, na hatua mpya ambazo hazikuwepo awali kwa wakimbizi na wahamiaji, na tunapaswa kufuria hilo, na kuliunga mkono.”