Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda na nuru kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Uganda na nuru kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini kwa miaka miwili na nusu sasa hali si shwari tangu kuzuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwezi Disemba mwaka 2013. Nuru ya kupatikana amani ilianza kuonekana mapema mwaka huu baada ya makubaliano yaliyowezesha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa, Hata hivyo mwezi uliopita mapigano mapya yameibua wakimbizi na hivyo kuongeza idadi ya raia wanaosaka hifadhi nchi jirani ikiwemo Uganda.

Miongoni mwa ambao walishakimbilia Uganda ni Esther na wanawe ambao wameanza kuonea ahueni baada ya serikali ya Uganda kuchukua hatua. Je ni nuru gani hiyo? .Na maisha yako vipi? Ungana basi na Flora Nducha kwenye makala hii.