Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi hospital Quetta, Pakistan

Ban alaani shambulio la kigaidi hospital Quetta, Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la bomu la kigaidi lililofanyika leo kwenye hospitali ya kiraia mjini Quetta,jimbo la Balochistan nchini Pakistan.

Ban amesema shambulio hilo lililowalenga waombolezaji kwenye hospitali hiyo ni la kutisha na kusikitisha sana.

Katibu Mkuu ameitaka serikali kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha usalama wa watu wake na kuwafikisha wahusika wa shambulio la leo kwenye mkono wa sheria.

Ametoa salamu za rambirambi kwa wahanga na familia za waliopoteza maisha huku akiwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushikamana na watu na serikali ya Pakistan. Duru zinasema watu takriban 70 wamepoteza maisha kwenye shambulio hilo la kigaidi.